BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

 

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

 

IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU.

 

UHAKIKI WA DINI NO.3

 

UHAKIKI WA DINI KUPITIA MSINGI WA IJTIHADI.

 

Katika makala iliyopita, tulielezea umuhimu wa uhakiki wa dini kupitia msingi wa Ijtihadi, katika makala hiyo tulielezea misingi mitatu inayoweza kumuongoza mwanaadamu katika uhakiki wake wa dini, katika makala hii tutaendelea kuelezea misingi mengine ya

 

 

 

uhakiki wa dini.

 

 

6. Mijengeko na miundo mingi inayotokana na harakati mbalimbali, kumbukumbu, utajo, kiriri, upangaji wa mipango tofauti na mienendo mbalimbali inayoonekana katika jamii, siasa n.k. ni mitazamo na akida zinazotokana na tata au kasumba zinazohusiana

 

na falsafa za dini. Kwa hiyo kama kuna ulazima wa kufanya harakati za kisiasa na kijamii, basi vilevile kuna ulazima kwa kitengo cha Hizbullahi kutumia nguvu alizonazo kadri ya uwezo wake kwa ajili ya kupingana na kukabiliana na kasumba hizo, na njia

 

bora ya kukabiliana na kasumba hizo ni kutaalamika kielimu na kuweza kuzihalili na kuzijibu tata hizo kwa kutumia elimu ya dini na mitazamo inayokubalika kiakili. Kwa hiyo jambo linalowapasa Waislamu kulifanya ni kufahamu chanzo cha tata na kasumba

 

hizo, njia wanazotumia, na mipango inayopangwa na watu wa nchi za kimagharibi kwa ajili ya kuiharibu dini tukufu ya Mwenyeezi Mungu.

 

Katika paragrafu hii sio vibaya kulifafanua neno kasumba.

 

Kasumba ni mabadilisho ya fikra za mtu yanayosababishwa na elimu au utamaduni wa jamii, yanayomfanya afuate mwenendo usio muafaka na utamaduni wake au utu wake wa asili, kwa mtazamo mwengine, kasumba ni mabaki ya fikra za kikoloni katika

 

kichwa cha mtu akiamini na kutenda mambo yanayooana na tabia za kikoloni.

 

7. Kuna umuhimu wa kutambua falsafa ya dini kwa sababu, kwa mtazamo wa kielimu na kimantiki mwanaadamu ni kiumbe anayependa kudadisi na kutafuta uhakika wa mambo, na hii ina maana ya kuwa kila mwanaadamu anahitajia kujua mambo

 

yanayomletea faida, na kwa sababu hiyo basi, mwanaadamu hutafuta yale anayoyajua na yaliyo muhimu anayoyahitajia katika maisha yake ya kila siku. Hayo yalikuwa ni baadhi ya maelezo tu yanayohusiana na umuhimu wa falsafa ya dini.

 

MWISHO